Mamilioni ya watu walifurika katika mitaa ya mji mkuu wa Tehran kushiriki mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na baadhi ya wanafamilia wake waliouawa na kufikia daraja ya shahada.

6 Julai 2026 - 14:12

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA – Mamilioni ya waombolezaji walijitokeza katika mji mkuu wa Tehran kushiriki mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na baadhi ya wanafamilia wake waliouawa pamoja naye na kufikia daraja ya shahada.

Dunia Yashuhudia Mamilioni ya Waombolezaji Wakimzika Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei +Picha

Maelfu kwa maelfu ya waombolezaji walifurika katika barabara kuu za jiji hilo, huku Barabara ya Azad ikishuhudia umati mkubwa wa watu waliokusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo. Waombolezaji walionekana wakionesha huzuni kubwa, wakibeba picha na mabango mbalimbali pamoja na kuimba kaulimbiu za kuenzi mchango wake kwa Uislamu na Umma wa Kiislamu.

Taswira zilizorekodiwa kutoka Barabara ya Azad zinaonyesha bahari ya watu waliokusanyika kwa ajili ya kushiriki ibada ya kuaga na mazishi ya kiongozi huyo, ambaye wafuasi wake wanamuelezea kuwa alitumia maisha yake yote katika kuitumikia dini ya Uislamu, kuutetea Umma wa Kiislamu na kusimama upande wa wanyonge na wanaodhulumiwa.

Dunia Yashuhudia Mamilioni ya Waombolezaji Wakimzika Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei +Picha

Mazishi hayo yameelezwa kuwa miongoni mwa makusanyiko makubwa zaidi ya waombolezaji katika historia ya hivi karibuni ya Iran, huku watu kutoka maeneo mbalimbali wakihudhuria kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu na kuonesha mshikamano wao na familia yake pamoja na taifa la Iran.

Your Comment

You are replying to: .
captcha